Tuesday, January 10, 2012

UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI KUKAMILIKA KWA SHILINGI BILION 214.6


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhani Dau akitia saini ili kuruhusu Mradi wa Daraja la Kigamboni kuanza.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau, alisema Shirika la NSSF itachangia asilimia 60, wakati serikali itachangia asilimia 40.

“Kunakila sababu ya kukamilisha mradi wa daraja kwa wakati hii nikutokana na kuwepo tayari kwa pesa za mradi, ni matumaini yangu mradi utafanikiwa kwa wakati na watanzania kushuhudia ndoto ya ujenzi wa daraja imekamilika” alisema
Alisema licha ya kusaini mkataba huu kama ishara ya kuanza kwa mradi zipo changamoto nyingi lakini baadhi ya changamoto ni kwa upande wa kurasini kuna kiwanja kinjamatatizo, vile vile baadhi ya makutano ya barabara ya Chang’ombe , Kamta na Tazara ktuokana na foleni kubwa lakini haya yote tunaimani serikali itayapatia ufumbuzi wa haraka.....


Serikali kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), leo imetia saini na Kampuni ya Kichina, China Railway Jiangchang Engeneering CO. Ltd kama ishara ya kutekeleza ujenzi wa mradi wa daraja liakalo unganisha wakazi wa Kigamboni na Dar es Salaam utakaogharimu zaidi ya Shilingi bilion 214.6 kwa muda wa miezi 36.






No comments:

Post a Comment