Tuesday, January 10, 2012

WAKAZI WA UINGEREZA WALIVYOCHANGIA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO TANZANIA


 Picha ya pamoja baada ya shughuli kuisha na baadhi ya wadau waliojitokeza kuchangia.
------
Salaam,
SIKU ya Jumamosi tarehe 7 Januari 2011 Serengeti Freight wakishirikiana na Miss Jestina Blog pamoja na Urban Pulse walifanya harambee maalum ya kuchangia Watanzania walioathirika na mafuriko yaliotokea hivi karibuni mwishoni mwa mwaka jana nyumbani Tanzania.

Mgeni rasmi alikuwa Naibu balozi, Mh Chabaka Kilumanga. Mh Balozi aliongea na kushukuru Watanzania wote walioguswa na kujitolea kwa hali na mali ili kuweza kusaidia Watanzania wenzao waliokumbwa na janga hili. Misaada bado inaendelea kupokelewa na kukusanywa mpaka mwisho wa mwezi huu. Hivyo basi kwa wale wote walioshindwa kuweza kufika siku ya Jumamosi kutoa michango bado nafasi ipo.Kumbuka hili ni janga letu wote tafadhali fanya sehemu yako kwa jinsi Mungu anavyokubariki. 

No comments:

Post a Comment