Monday, January 9, 2012

JK Vs SLAA: UNGEMCHAGUA NANI?



Zaidi ya mwaka mmoja umeshapita sasa tangu Rais Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani katika muhula wake wa pili wa kuliongoza taifa hili. Ingawa mwaka mmoja sio muda wa kutosha kwa kiongozi kukamilisha malengo na ahadi zote,ni muda wa kutosha kutoa picha ya mfumo na mtindo wa ki-uongozi.
Je,mwaka mmoja baadae,uchaguzi ungefanyika unadhani kura yako ungempa nani katika ya Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita,Dr.Wilbrod Slaa?Kwanini?
Ninapoandika post hii, Dr.Wilbroad Slaa,kupitia tamko la CHADEMA wametoa msimamo wao kuhusu uongozi wa Rais Kikwete mwaka mmoja baadae.Gazeti la Mwananchi limeandika kwa kirefu kuhusu hilo na unaweza kulisoma kupitia hapa.
NB: Unaweza kutumia fursa hii kutoa maoni ya kujenga kwa maana ya kwamba kutoa maoni yenye tija na sio lawama na matusi.

No comments:

Post a Comment